jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limewatia mbaroni watu watatu ambao walikamatwa
wakiwa na bunda kumi za karatasi zenye sura ya Dora mia moja ambapo
kila bunda moja lina karatasi 86 zenye thamani ya shilingi milioni 86 za
kitanzania .
Watuhumiwa waliokamatwa wametajwa
kuwa ni Bonifasi Simwanza(41) ambaye ni raia wa nchi ya Zambia, Adam
Msongole(26)mkazi wa mji mdogo wa Tunduma uliopo wilayani Momba mkoa wa
Mbeya uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia na Hatmani Steven(29) Mkazi
wa eneo la Makumbusho kijitonyama jijini Dar es salaam.
Akizungumza
Leo ofisini kwake kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela
alisema kuwa tukio hilo lilitokea April 19 mwaka huu majira ya saa 7
mchana huko katika eneo la Mtaa wa Oil Com Petrol station mjini kati manispaa ya songea.
Alieleza
zaidi kuwa siku hiyo ya tukio Afisa upelelezi wa makosa ya jinai wa
mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi akiwa ameongozana na askari walifanikiwa
kuwakamata watu watatu wakiwa na karatasi za kutengenezea noti bandi.
Alifafanua zaidi kuwa askari hao walikamata bunda kumi za karatasi zenye sura sawa na dola mia moja ambapo kila
bunda moja lina karatasi 86 na baadhi ya vitu vingine ambavyo alivitaja
ni mkasi mmoja, Gloves mbili na pamoja na karatasi nyeusi ambazo
zinadaiwa kuwa ni malighafi za kutengenezea dola.
Kamanda
Msikhela alieleza kuwa jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kufanya
uchunguzi wa kina na baada ya kukamilisha uchunguzi huo watuhumiwa
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


0 comments:
Post a Comment