![]() |
| Uchunguzi wa vinasa sauti za safari ya ndege unaendelea |
''Nguvu kutoka nje'' ndio
iliyosababisha ajali ya ndege iliyoanguka katika rasi ya Sinai na kuua
watu 224 wengi wao raia wa Urusi.
Kogalymavia, Kampuni inayomiliki
ndege hiyo ya Urusi imesema hakuna njia nyengine ya kuelezea ajali hiyo
mbaya zaidi katika miaka ya hivi punde.
Katika mkutano na
wanahabari jijini Moscow, afisa mmoja mkuu wa shirika hilo Kogalymavia
alipinga madai kuwa ndege hiyo ilikuwa na hitilafu au makosa ya rubani.
![]() |
| Watu wote 224 waliokuwa katika ndege hiyo waliaga dunia. |
Aidha msemaji wa kampuni hiyo amekiri kuwa ndege hiyo ilikuwa na
hitilafu kwenye bawa lake lakini wahandisi waliirekebisha kabla ya ndege
hiyo kupaa kutoka Sharm el-Sheikh kuelekea St Petersburg.
Kogalymavia ambayo ndege yake ilianguka katika rasi ya Sinai nchini Misri imekanusha kuwa hiyo ndio chanzo cha ajali hiyo mbaya.
Sasa
mtaalamu wa maswala ya usalama wa ndege nchini Urusi sasa anasema kuwa
kuna uwezekano lilikuwa shambulizi la kigaidi ndilo lililosababisha
ajali hiyo ya ndege.
Alexander Smirnov anasema kuwa inashangaza kuwa ndege hiyo ilipoteza kasi ilhali marubani wote hawakujaribu kutafuta msaada.
![]() |
| Mtaalamu wa maswala ya usalama wa ndege nchini Urusi sasa anasema kuwa kuna uwezekano lilikuwa shambulizi la kigaidi |
Matamshi hayo ya Smirnov yanatoekea huku uchunguzi wa vinasa sauti vya ndege hiyo ukiwa bado unaendelea.
Awali,Miili
ya watu 160 waliofariki dunia katika ajali ya ndege eneo la Sinai
nchini Misri iliwasili mjini St Petersburg nchini Urusi
Watu wote 224 waliokuwa katika ndege hiyo waliaga dunia.
![]() |
| Kogalymavia, Kampuni inayomiliki ndege hiyo ya Urusi imesema hakuna njia nyengine ya kuelezea ajali hiyo |
Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi amewataka watu wote wawe na uvumilivu wakati uchunguzi ukiendelea.
Mmoja
wa wachunguzi wa masuala ya safari za ndege kutoka Urusi amesema kuwa
ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai nchini Misri ilivunjika
ikiwa hewani.
Aleksandr Neradko amesema kwamba mabaki ya ndege hiyo yametapakaa katika rasi ya Sinai.
![]() |
| Urusi:'Nguvu kutoka nje'ilisababisha ajali ya ndege |
Wengi wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo ni raia wa Urusi.
Mchunguzi kutoka nchini Urusi amesema kwamba ni mapema mno kujua chanzo cha ajali hiyo.
Wapiganaji
wa kundi la Kiislamu la Islamic State walikuwa wamedai kudungua ndege
hiyo, madai ambayo yamepingwa na serikali za Urusi na Misri.






0 comments:
Post a Comment