| Elizabeth Kinyami anayedaiwa kumtoroka mumewe. |
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini Robert
alifiwa na mkewe wa kwanza ambaye alizaa naye watoto wawili, lakini
wakati akiwa naye, alikuwa akichepuka na Elizabeth, hivyo baada ya
mwenzake kutangulia mbele ya haki, alimchukua mchepuko wake na kuishi
naye kinyumba.
Inadaiwa kuwa baada ya kuishi kama mke
na mume kwa miaka miwili, msichana huyo alimwambia Robert kuwa amepata
chuo cha kusoma mjini Tanga, ambapo mwanaume alikubali na kumsaidia ili
aendelee na masomo
.
.
Muhula wa masomo ulipoisha, Robert
alimtumia nauli ili arejee, lakini katika hali ya kushangaza, hakurudi
licha ya kutumiwa mara tatu, kabla ya mwanaume huyo kuamua kumfuata na
alipofika huko ndipo alipobaini kuwa alikuwa akiishi na mwanaume
mwingine.
| Mume anayedaiwa kutorokwa na mkewe. |
“Ni kweli Eliza ni mke wangu,
nimemsaidia kumtafutia chuo lakini ukweli ni kwamba alikuwa ananilaghai,
kumbe alikuwa na mambo yake, nimemgharamikia sana ikiwemo mawigi,
mikoba na vitu vingine akidai anaenda chuo Tanga, kumbe alikuwa na
mwanaume mwingine,” alisema Robert alipotakiwa kutoa ufafanuzi.
Kwa upande wake, Elizabeth alisema madai
hayo siyo ya kweli, kwani Robert anauelewa ukweli wa suala lake, bali
yeye aliwahi kumfumania mwenzake mara nyingi.“Kuhusu hili suala, yeye
analijua mwanzo mwisho, nitamtafuta ili tuzungumze,” alisema mwanamke
huyo.

0 comments:
Post a Comment