Mwanamke mmoja wa kipalestina
amekufa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa shambulio mwezi Julai
lililomuua mumewe na mtoto wao mdogo wa kiume.
Riham Dawabsha
alikua anauguza majeraha ya kuungua kiasi cha asilimia tisini ya mwili
wake aliyoyapata baada ya nyumba yao kupigwa na mabomu ya moto katika
kijiji cha Duma kilichopo katika ukingo wa magharibi .
Mtoto wake wa miezi 18 aliuawa katika shambulio hilo pamoja na mumewe ambaye alikufa hospitalini wiki moja baadaye .
Mtoto mwingine wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne bado anapata matibabu ya majeraha.
Shambulio hilo lililaaniwa na jamii ya kimataifa na kusababisha maandamano makubwa ya wapalestina
Maafisa
wa polisi nchini Israeli waliwakamata watu 7 wanaoshukiwa kuvamia
nyumba hiyo ya mpalestina katika ukingo wa magharibi na kuiteketeza
moto.




0 comments:
Post a Comment