![]() |
| MEYA WA MANISPAA YA SONGEA CHARLES MHAGAMA |
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Charles Mhagama
(50) anayekabiliwa na shtaka la rushwa kinyume na kifungu cha namba
15(1) B cha sheria ya uzuiaji na upambanaji wa rushwa namba 11 ya mwaka
2007 amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama ya Wilaya ya Songea kujibu shtaka la rushwa linalomkabili
Katika Mahakama hiyo iliyokuwa imefulika watu waliokuja kusikiliza kesi
hiyo waendesha Mashtaka wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
Rushwa (TAKUKURU)mkoani Ruvuma Chali Kadege na Helman Malima mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Elizabeth Missana walisoma hoja
14 za maelezo ya awali ambapo hoja ya kwanza mshitakiwa Charles Mhagama
(50)ambaye ni Diwani wa kata ya Matogoro manispaa ya Songea.
Walisema kuwa hoja ya pili baadhi ya majukumu yake kama diwani
mshitakiwa kama diwani ni kuwawakilisha wananchi wa kata yake katika
baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa hiyo na kwamujibu wa
majukumu yake ya udiwani mshitakiwa Mhagama ni mwenyekiti wa kamati ya
maendeleo ya kata.
Walieleza zaidi mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Mhagama alijenga nyumba
pembeni ya ofisi ya kata ya matogoro katika eneo la kata hiyo ambapo
ofisi mpya ya kata ilishajengwa na mwaka 2010 mshitakiwa Mhagama
alimfuata Shaib Ngonyani na akamweleza kuwa yeye ndiye anayejenga nyumba
kwenye eneo la ofisi ya kata ya Matogoro.
Walifafanuwa zaidi kuwa mwaka 2011 mshitakiwa alianza kujenga nyumba
pembeni ya ofisi ya kata ya Matogoro na manamo mwezi wa 12 mwaka 2011
kuliitishwa mkutano na ofisi ya kata ya Matogoro na diwani huyo
alikuwepo na alipewa malalamiko ya ujenzi wa nyumba kwenye eneo la ofisi
ya kata.
Mawakili hao wasomi wa TAKUKURU waliendelea kutoa hoja za awali
mahakamani hapo kuwa mwaka 2011 wananchi wenye hasira walibomoa nyumba
aliyokuwa anajenga nyumba na baadae alienda kushitaki polisi ambapo
polisi wakishilikiana na yeye walikwenda kuwakamata Mohamed Mvula na
Seif Abdlah .
Walisoma hoja nyingine kuwa mshitakiwa alimuomba Shaibi ngonyani
amuandikie hati ya mauziano ya eneo ambalo yeye alikuwa anajenga nyumba
ambapo mwaka 2010 alimshawishi Shaibu Ngonyani kwa kumpa kiasi cha sh.
250,000/=ambayo aliitoa kwa nyakati tofauti mpaka ilipotimia.
Waliieleza mahakama kuwa mshitakiwa Mhagama alimwambia Ngonyani kuwa
hela hiyo ni ya chai kwani nyumba ameshajenga hivyo hakuna mtu yeyote
atakaye mshitaki ,wakati anajenga nyumba hiyo tayari ofisi ya kata
ilikuwa imeshajengwa na hiyo kata Mhugama ndiye diwani na haliweza
kumshawishi Ayubu Singwa awe shahidi wa siku ambayo ngonyani
alimwandikia hati ya mauziano.
Hata hivyo mshitakiwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Matogoro
alikubaliana na hoja sita alizosomewa kati ya hoja 14 zilizosomwa
mahakamani hapo ambapo aliongozwa na wakili anayemtetea wa kujitegemea
Abel Ngilangwa na upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wawili
ulidai kuwa wanatarajia kuleta mashaidi 13 na vielelezo 4 na kwamba kesi
hiyo imehairishwa hadi 15 mei mwaka huu.


0 comments:
Post a Comment