Ugonjwa wa homa ya Lassa Afrika
Magharibi unaelezwa kusahaulika kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola
na Wahudumu wa afya wamesema huenda wakakosa rasilimali kukabiliana na
ugonjwa huo iwapo utakithiri.
Awali dalili za homa hii zilionekana
kama za ugonjwa wa ebola.kuvuja damu, kutapika na joto kali la
mwili.lakini kwa kuwa ebola ni ugonjwa mpya, homa ya Lassa nayo bado
ipo, ambayo inaelezwa kuwa kila mwaka watu 300,000 mpaka 500,000
huathiriwa na homa hii na watu mpaka 20,000 hupoteza maisha.
Kila
nchi iliyoathiriwa na ebola pia ina ugonjwa wa homa ya Lassa, ijumaa
juma lililopita Dr.Geraldine O'Hara kutoka Shirika la Madaktari wasio na
mipaka MSF ameiambia BBC kuwa mmoja wa wafanyakazi wenzake alipoteza
maisha ingawa walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake.
Inaelezwa
kuwa Nigeria huenda ikakumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Lassa, wakati
huu ikiwa ni majuma kadhaa baada ya kufanikiwa kukabili ugonjwa wa
ebola.
Kuna tofauti moja kubwa kati ya ebola na homa ya
Lassa.Lassa husababishwa na Panya ambao hubeba vijidudu kwenye maeneo ya
makazi ya watu na kwenye hifadhi za vyakula hasa kipindi cha Kiangazi.
Profesa
Robert Garry kutoka Chuo cha Tulane amefanya utafiti kuhusu ugonjwa huu
kwa amesema Kumekua na ripoti kadhaa za watu kuugua homa ya Lassa
nchini Sierra Leone.
Lassa huambukiza lakini si kila anayeambukizwa huwa katika hali mbaya, ugonjwa huu hausambai kwa kasi kama ebola


0 comments:
Post a Comment