Takriban watu 24 wamepoteza maisha
na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya Boti inayoelezwa kubeba
wahamiaji kuzama baharini mjini Istanbul nchini Uturuki
Ajali hiyo imetokea katika eneo bahari Nyeusi na bahari ya Marmara zinapokutana.
Operesheni ya uokoaji angani, baharini na chini ya bahari inaendelea miili mingi ikiripotiwa kuibuliwa kutoka majini.
Operesheni
ya baharini ina changamoto ya kuwepo kwa upepo mkali , mmoja wa
waokoaji Ali Saruhan amesema Boti hiyo ni ndogo lakini ilibeba watu 40
akieleza kuwa ameshuhudia miili ya watoto ikielea baharini.
Uraia
wa wahamiaji hao bado haujajulikana, vyombo vya habari vinasema ni
aghalab kwa chombo kilichobeba wahamiaji kuwa katika eneo hilo.
Mwandishi
wa BBC anasema Uturuki ni moja ya vituo vikuu kwa wahamiaji wanaosafiri
kwenda nchi za ulaya, lakini wengi wao husafiri kupita bahari ya Aegean
mpaka Ugiriki.
Boti zinazowasafirisha wahamiaji hao hujaza
wasafiri kupita uwezo wake, huku wahamiaji hao wakilipa nauli ya maelfu
ya dola kwa ajili ya kusafirishwa.
Miezi miwili iliyopita kundi
la wahamiaji, wengi wao raia wa Syria na Afghanistan waliokolewa eneo la
kaskazini mwa pwani ya Bahari mjini Istanbul wakiripotiwa kwenda nchi
za ulaya.


0 comments:
Post a Comment