![]() |
| Masanduku ya kura nchini Nigeria |
Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi
wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu
cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye
madarakani, Goodluck Jonathan.
Lakini majimbo ya kusini yenye
idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayajatangaza matokeo
na mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali.
Tume
ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne
asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku
hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la
kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu
chafu.


0 comments:
Post a Comment