![]() |
| MAREHEMU ABDU BONGE |
Jioni ya March 28, tulipokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi na
muanzilishi wa Tiptop Connection Abdu Bonge lenye wanachama kama Tunda
Man, Madee, Dogo Janja na wengine waliopita kama Keisha, Cassim Mnganga
na MB Dogg.
Jioni ya March 28 2015 ndio taarifa zilianza kusambaa lakini chanzo
cha kifo cha ghafla cha Abdul hakikuwa kimesemwa lakini mdogo wake ambae
ni Babu Tale ameongea kusema
‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu,
wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya
tatu akasema ngoja aende, Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna
mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie
kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema
Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa
kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia
kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese wakasema ameshafariki‘ – Babu Tale.
Mwili wa marehem umesafirishwa leo hii baada ya kuzuiliwa mpaka
uchunguzi ulipokamilika.maziko yatafanyika kijiji cha Mkuyuni Morogoro,
kwa asiyepajua Mkuyuni ni njia ya kwenda Matombo. #RIP #AbduBonge


0 comments:
Post a Comment