![]() |
| Meli za ulinzi za Urusi |
Urusi imeanza kuruhusu askari kutoka nje wenye utalaam ili kuingia katika jeshi lake.
Hata hivyo, wataalam wa Urusi wanasema hatua hiyo haina uhusiano wowote na mgogoro nchini Ukraine.
Rais
Vladimir Putin ameidhinisha sheria inayowawezesha raia wa kigeni
kufanyakazi angalau kwa miaka mitano katika jeshi la Urusi ili mradi
wanajua kuzungumza Kirusi.
Wataalam hao wanatarajiwa zaidi watatoka katika jamhuri za Asia ambazo awali zilikuwa sehemu ya muungano wa nchi za Soviet.
Wageni
wa kujitolea, wakiwemo Warusi wamekuwa wakipigana nchini Ukraine. Hata
hivyo Urusi imekuwa ikikana kupeleka majeshi yake huko.
Serikali
ya Ukraine na nchi za magharibi wanasema Urusi imetuma silaha nzito na
askari wenye utaalam wa hali ya juu kuwasaidia watu wanaotaka kujitenga
mashariki mwa Ukraine.


0 comments:
Post a Comment