![]() |
| Taliban yaua wanafunzi Pakistan |
Takriban watu ishirini wameuwawa
wakiwemo watoto na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa
Taliban kuvamia shule moja inayosimamiwa na jeshi kaskazini - magharibi
mwa Pakistan.
Wakuu katika jimbo la Peshawar wanasema kwamba
wapiganaji watano au sita hivi wenye silaha waliingia katika Shule hiyo
iliyo na wanafunzi 500.
Walinda usalama wa Pakistan kwa sasa wamezingira jumba hilo huku milio ya risasi ikisikika.
Operesheni hiyo kali inaendelezwa ilikuwanusuru wanafunzi .
Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa.


0 comments:
Post a Comment