![]() |
| Ndugu na jamaa wana imani ya kuwapata wapendwa wao |
Polisi nchini Mexico wamepambana na
Waandamanaji walioandaa tamasha mjini Chilpancingo wakikumbuka kundi la
Wanafunzi 43 waliopotea zaidi ya miezi miwili iliyopita.
Polisi wamesema maafisa kadhaa wamejeruhiwa, wakiwemo baadhi waliogongwa na gari.
Makundi hayo mawili yameshutumiana kuanza machafuko siku ya jumapili.
Tukio la kupotea kwa Wanafunzi, mmoja kati yao kuokotwa akiwa amepoteza maisha, kulizua maandano sehemu zote nchini Mexico.
Vurugu zilijitokeza baada ya Waandamanaji kuweka vizuizi katika mtaa mjini Chilpancingo kabla ya tamasha lililopangwa kufanyika.
Tamasha liliahirishwa baada ya vurumai hizo,wakati huo,magari kadhaa yalichomwa moto.
Kundi
la Wanafunzi 43 kutoka taasisi ya mafunzo ya ualimu mjini Ayotzinapa
lilitoweka tarehe 26 mwezi Novemba baada ya kupambana na Polisi wa
manispaa ,mjini Iguala.
Inadaiwa kuwa wanafunzi 43 walichomwa moto
katika jalala la takataka baada ya kubaini kuwa wanafunzi hao walikuwa
kwenye kundi hasimu.
Uchunguzi uliofanywa kwa mfupa uliookotwa
kwenye mto karibu na jalala umeonyesha kuwa ni Kiungo cha mmoja wa
Wanafunzi 43 waliopotea.
Ndugu wa Wanafunzi hao wamesema hawatakata tamaa wakiwa na matumaini kuwapata.


0 comments:
Post a Comment