![]() |
| Wafanyakazi wa Afya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakihudumia wagonjwa |
Wafanyakazi wa afya 81 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewasili nchini Guinea, kusaidia kukabiliana na janga la Ebola.
Timu hiyo ni pamoja na madaktari, wauguzi, wataalam wa maabara, saikolojia na mawasiliano.
Wataalamu hao wataanza kazi moja kwa moja katika vitengo husika na kutibu ugonjwa wa Ebola nchini Guinea.
Pia
watatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa mitaa ya nchi hiyo kuhusu
namna ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola nchini humo.
Wakati
huo huo Shirika la Afya Duniani limetoa takwimu mpya za mlipuko wa
Ebola. Kwa mujibu wa shirika hilo vifo vilivyotokana na Ebola katika
nchi tatu zilizoathirika zaidi imepita watu 8,000.
Takwimu hizo
mpya ni kwa nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia pekee. Watu 8,153
wameripotiwa kufa, ambapo watu 20, 656 wameugua ugonjwa huo katika nchi
hizo tatu.
Takwimu zinaonyesha kuwa Sierra Leone - imekuwa na
wagonjwa 9,772 na vifo 2,915. Liberia wagonjwa 8,115 na vifo 3471 ambapo
Guinea imeripotiwa kuwa na wagonjwa 2,769 na vifo 1,767.
Takwimu
hizo ni hadi kufikia Desemba 31 kwa upande wa Liberia, na kwa upande wa
nchi za Sierra Leone na Guinea takwimu hizo ni hadi Januari 3, 2015.
Pia nchini Mali kuna taarifa za wagonjwa 8 na vifo vya watu 6. Ambapo Uingereza ina mgonjwa mmoja na hakuna kifo.


0 comments:
Post a Comment