![]() |
| Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa |
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa
wito kwa rais wa Rwanda, kuwa mvumilivu huku uhasama kati yake na nchi
jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ukiendelea kutokota katika
maeneo ya mipakani.
Bwana Ban, alizungumza na rais Paul Kagame baada
ya serikali yake kuishutumu Congo, kwa kufanya shambulio katika ardhi
yake makusudi na kumuua mama mmoja na kumjeruhi mtoto wake.
Msaidizi
wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa, amenukuliwa akiiambia Umoja wa
Mataifa kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa M23, wameonekana wakirusha
makombora wakilenga Rwanda.
Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeshutumu
Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao wa M23, madai ambayo yamepingwa
vikali ya utawala wa Kigali.
Wanajeshi wa Congo wakishirikiana na wanajeshi
wa Umoja wa Mataifa, wamekuwa wakifanya mashambulio dhidi ya waasi hao
wa M23 karibu na mpaka wa Rwanda, tangu wiki iliyopita
![]() |
| Wanajshi wa Umoja wa Mataifa nchini DRC |
Waasi walengwa na UN
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kutunza amani
nchini DRC, Monusco, kiliimarishwa zaidi pale wanajeshi elfu tatu zaidi
walipotumwa nchini humo kupambana na waasi hao.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise
Mushikiwabo, amesema mabomu na makombora kumi na tatu yalirushwa katika
ardhi yake siku ya Jumatano na mengine kumi siku ya Alhamisi.
Waziri huyo amedai kuwa kufikia sasa wanajeshi hao wa Congo wamefanya mashulio thelathini na nne nchini Rwanda.
Amewashutumu wanajeshi wa DRC kwa kuwalenga raia
wake na kusisitiza kuwa kwa sasa wanajiepusha kulipisa kisasi lakini
hawatasita kujibu ikiwa uchokozi huo hautakoma.
Msemaji wa jeshi la Congo Kanali Olivier Hamuli
ameiambia BBC kuwa jeshi lake haliwezi kurusha makombora kulenga maeneo
yanayokaliwa na raia.
''Waasi ndio wanaoweza kufanya kitendo kama
hicho, wapiganaji wa M23 na wala sio wanajeshi wake ndio waliokuwa
katika eneo ambalo makombora hayo yalirushwa'' Alisema Kanali Hamuli.
Matamshi hayo yaliungwa mkono na msaidizi wa
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Mulet ambaye aliiambia Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, wanajeshi wake nchini DRC walishuhudia
wapiganaji wa M23, wakirusha makombora wakilenga Rwanda na wala sio
wanajeshi wa Congo.
Takriban watu laki nane wamekimbia makwaoi
nchini Congo tangu waasi hao wa M23 kuanzisha mashambulio katika eneo la
Mashariki mwa Congo Aprili mwaka wa 20120



0 comments:
Post a Comment