Uingereza huenda ikaanzisha mashambulio dhidi ya utawala wa Syria, bila kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Hayo ni kwa mujibu wa ushauri wa wataalamu wake wa masuala ya kisheria.
Ushauri
huo unasema, mashambulio hayo yatahitajika ikiwa yatatekelezwa ili
kuzuia raia kuuawa, hata ikiwa wanachama wa kudumu wa baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa Urussi na Uchina
zikitumia kura zao za turufu
kupinga mikakati za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria.
Maafisa wa ujasusi nchini Uingereza wamemueleza
Waziri Mkuu, David Cameron kuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa serikali ya
Syria ilihusika na shambulio la kemikali wiki iliyopita mjini Damascus.
Wabunge wa Uingereza wanatarajiwa kujadili suala hilo katika kikao chao cha leo jioni.
Serikali ya Syria imekana madai ya kutumia
silaha za kemikali katika shambulio mjini Damascus tarehe 21 mwezi huu,
ambapo mamia ya watu waliuawa.
Lakini Bwana Cameron anaamini kuwa kuna ushahidi
wa kutosha kutoka wa maafisa wake wa ujasusi na pia kutoka kwa
wanainchi kuhusu ukatili unaofanywa na utawala wa sasa wa Syria.
Ofisi ya Waziri mkuu wa Uingereza, imechapisha
ripoti hiyo, kuambatana na ushauri wa mkuu wake wa sheria Dominic
Grieve, inayotoa idhini ya mashambulio ya kijeshi ili kuzuia utumiaji wa
silaha za kemikali siku zijazo, kuambatana na sheria za kimataifa


0 comments:
Post a Comment