Takriban wahamiaji 700 walokuwa wanajaribu kusarfiri kwa boti
kutafuta maisha bora Ulaya wanahofiwa wamefariki pale boti yao ilipozama
nje ya pwani ya Libya.
Maafisa wa usalama wanasema watu 28 wameokolewa na miili 24
imegunduliwa lakini mamia ya watu hawajapatikana bado katika ajali
inayosemekana ni mbaya kabisa ya kutoweka kwa wahamiaji katika bahari ya
Mediterranean.
Meli ilizama km 193 kusini mwa kisiwa cha Utaliana cha Lampadusa,
wakati inaaminika wahamiaji walikwenda upnde mmoja wa boti wakati meli
kubwa ya mizigo ilikuwa inapita karibu yao.
Viongozi wa Ulaya wametoa wito wa kuchukuliwa hatua za mara moja
kutanzua mzozo wa wahamiaji wakati maelfu ya watu kutoka Afrika na
Mashariki ya Kati wanajaribu kukimbia kutokana na ufukara, vita na
vurugu la kisiasa linalosababisha ukosefu wa usalama katika nchi za
kiarabu. Watu hao wanasongamana katika boti na kujaribu kuvuka bahari ya
Mediterranean , kuelekea hasa Utaliana.
Mkuu wa masuala ya Kigeni ya Umoja wa Ulaya Federica Mogherini
anasema “ Tumesema mara nyingi sana, isipate kutokea tena, huu ni wakati
wa Umoja wa Ulaya kukabiliana na maafa haya bila ya kuchelewa.”
Waziri Mkuu wa Utaliana Matteo Renzi anasema vidadi ya vifo bila
shaka inatazamiwa kuongezeka akiuliza, “inakuwaje tunashuhudia maafa
haya kila siku?”
Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema ni lazima kwa maafisa
kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu inyosababisha vifo
vya zaidi ya watu elfu nne katika bahari ya Mediterranean wanaojaribu
kutafuta maisha bora Ulaya.
Maelfu ya wahamiaji wengi wao kutoka maeneo yenye vita Afrika na
Mashariki ya Kati wanafanya safari ya hatari kubwa kuvuka bahari ya
Mediterrean kwa matumaini ya kuwasili Ulaya.
Siku ya Ijuma Rais Barack Obama na mgeni wake Waziri Mkuu wa Utaliana
Matteo Rnezi walijadili suala la wahamiuaji wakati wa cmazungumzo yao
hapa Washington.


0 comments:
Post a Comment