![]() |
| Rais wa zamani Mohammed Morsi |
Makahama nchini Mirsi imemhukumu
aliyekuwa rais wa zamani Mohammed Mosri kifungo cha miaka 20 gerezani
kutokana na kuuawa kwa waamdamanaji wakati akiwa madarakani.
Hii nidyo hukumu ya kwanza kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani, na moja moja ya hukumu zinazomuandama.
Mosri aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.
Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa
kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa
upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwishoni mwa mwaka
2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
![]() |
| Wafuasi wa Morsi |
Baadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11
waliuawa kwenye makabiliano, wengi kutoka kwa Muslim Brotherhood.
Kabla
ya kutolewa hukumu ya leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa
Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.



0 comments:
Post a Comment