Huenda kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigera,
Abubakar Shekau aliuawa na maafisa wa usalama katika ufyatulianaji wa
risasi. Duru za kijeshi zinasema huenda Shekau aliuawa kati ya Julai 25
na Agosti 3.
Kundi la Boko Haram ambalo limekua likiendesha
maasi Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka wa 2009 halijatoa taarifa
yeyote. Marekani ilitangaza tuzo ya dola Milioni saba kwa yeyote yule
angepeana taarifa za kumnasa Shekau.
Shekau alipata majeraha mabaya na kuvukishwa
hadi katika mji ulioko mpaka na Cameroon kwa matibabu. Inaaminika
alikufa kati ya Julai 25 na Agosti tatu mwaka huu. Waandishi wa habari
wamesema hakuna taarifa huru ambazo zimethibitisha kifo cha Shekau.
Maelfu ya raia wameuawa tangu Boko Haram kaunza
maasi mwaka 2009. Abubakar Shekau alichukua uwongozi wa wapiganaji hao
wa kiisilamu baada ya kifo cha mwanzilishi wa Boko Haram, Muhammad Yusuf
aliyefariki dunia wakati akiwa kizuizini.
Kundi hilo limeendesha mashambulizi mabaya na ya
kikatili wakati wa uwongozi wa Shekau. Boko Haram wamekuwa
wakishinikiza kuunda taifa la Kiisilamu nchini Nigeria.
Hapo mwezi Mei mwaka huu Rais Goodluck Jonathan
alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskaizni mwa Nigeria
ambapo pia alituma jeshi kuendesha operesheni dhidi ya wapiganaji hao

