POWERBREAKFAST ya Clouds FM imefanya
uchambuzi wa story kubwa zote za kwenye kurasa za Magazeti Tz, kama
ulikuwa mbali na radio yako basi hapa unaweza kusoma na kusikiliza stori
zote zilizosikika hewani leo March 31.
Askofu Gwajima
amesema aliagiza bastola kwa ajili ya kujilinda, wasichana 3
wamekamatwa kwa kuhusishwa na ugaidi Kenya yumo Mtanzania, wadau
wanaotumia mitandao nchini wamepinga madai yaliyoidhinishwa kuhusu
muswada wa sheria ya makosa ya mtandao, wafuasi 25 wa CUF wavamiwa na
kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM, Serikali imetangaza
ugunduzi mpya wa gesi asilia huko Lindi, watu watano wanusurika kifo
baada ya ukuta wa jengo walilokuwa wakijenga kudondoka Mwanza, nauli
mpya za usafiri wa umma kujulikana mwishoni mwa wiki hii, Zanzibar
yakumbwa na uhaba wa Petroli na kuleta usumbufu kwa wananchi.
Kulikuwa na mahojiano na wafanyabiashara mbalimbali pamoja na Mkurugenzi wa jumuiya ya wafanyabiashara Steven Chamle ambao wamezungumzia mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea TZ.


0 comments:
Post a Comment