Leo hii Kilimanjaro Tanzania Music Awards KTMA, wameanza na kampeni ya wananchi kuanza kupendekeza majina ya nyimbo na wasanii wanaostahili kuingia katika kinyang'anyiro.unaweza kumpendekeza msanii/kikundi/video mara moja tu katika kipengele/category. Katika kipengele kimoja , unaweza kutuma mapendekezo matano tofauti (yaani kama wimbo bora wa mwaka, unaweza kupendekeza nyimbo mpaka 5 mradi ziwe tofauti)Pia unaweza kupendikeza msanii/wimbo/video moja katika vipengele tofauti (mfano, unaweza kupendekeza wimbo wa mwaka na pia ukapendekeza wimbo huo huo kwenye kipengele tofauti cha wimbo bora wa R&B)Ili kupendekeza kwa njia ya sms, tuma neno Kili au KTMA kwenda 15415 kisha fata maelekezaKupendekeza kwa njia ya whatsapp, save namba 0686528813 kwenye phonebook yako, kisha kupitia whatsapp, tuma neno Kili au KTMA kisha fuata maelekezo.Ila pia unaweza kupendekeza kwa kupitia mtandao ambao ni www.ktma.co.tz na kisha fuata maelekeza
0 comments:
Post a Comment