![]() |
| Mtuhumiwa wa mauaji ya jinai Germain Katanga |
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imempata na hatia ya uhalifu wa kivita mbabe wa kivita kutoka Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Germain Katanga.
Hata hivyo Katanga hakukutwa na hatia katika shtaka la udhalilishaji wa kijinsia.
Katanga ni mtu wa pili kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC
tangu ianzishwe mjini The Hague, Uholanzi mwaka 2002.Alituhumiwa kuhusika na mauaji ya wanavijiji zaidi ya 200 mwaka 2003 katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa dhahabu, kaskazini mashariki mwa Congo.
Katika shambulio hilo lililotokea mnamo Februari 24, 2003 watu 200 waliuawa katika kijiji cha Bogoro karibu na mpaka wa Uganda,Katanga wakati huo akiwa Kamanda wa kundi la waasi la Patriotic Resistance Force of Ituri (FRPI) lililotekeleza mauahi hayo.
Mwendesha mashtaka amesema nia yao kuu ilikuwa kuangamiza kijiji kizima.
Germain Katanga kwa jina la utani Simba alikanusha mashtaka hayo yote dhidi yake


0 comments:
Post a Comment