![]() |
| Wapenzi wa jinsia moja wanaishi maisha ya kujificha nchini Uganda. |
Rais wa Marekani Barrack Obama amemwonya rais wa
Uganda,Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini mswada wa sheria
inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja basi uhusiano kati ya Uganda na
Marekani utatatizika.
Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu
watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga
watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela.
Marekani ni mojawepo wa mataifa ya
kigeni yanayotoa kiwango cha juu zaidi cha msaada kwa Uganda, na mwaka
2011 idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani walitumwa kulisaidia jeshi la
Uganda kupanda na kundi la waasi wa Lords Resistance Army, LRA.
Lakini Rais Obama amesema uhusiano huo
unaodhaminiwa sana utatatizika zaidi iwapo mswada huo wa kupinga mapenzi
ya jinsia moja utaidhinishwa na kuwa sheria.
Ameeleza kwamba mswada huo ni wa kidhalimu na hatari kwa jamii ya mashoga nchini Uganda.
Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani,
Susan Rice, amesema kwenye mtandao wa Twitter kwamba amefanya mazungumzo
ya kina na rais Museveni jumamosi usiku kumtaka asitie saini mswada
huo.
Mbali na Uganda rais Obama amelalamika kwamba
visa vya mashambulizi na kuhangaishwa watu wanaoshiriki mapenzi ya
jinsia moja vimeenea katika mataifa kadhaa kutoka Urusi hadi Nigeria.


0 comments:
Post a Comment