![]() |
| Uharibifu wa Boko Haram |
Maafisa katika eneo la kaskazini mashariki mwa
Nigeria wanasema kuwa zaidi ya watu mia mmoja wameuwawa katika
shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko
Haram.
Shambulizi hilo katika kijiji cha Izghe katika
jimbo la Borno linajiri siku nne pekee baada ya watu 39 kuuwawa katika
shambulizi jingine.
Seneta
wa jimbo la Borno Mohammed Ali Ndume ameiambia BBC kwamba watu mia moja
na sita waliuwawa katika shambulizi hilo la hivi punde.
Amesema takriban wanamgambo mia moja walivamia
mji wa Izghe jumamosi usiku. Wananchi waliokuwa wakikimbia mashambulizi
hayo wamethibitisha kuwa takriban wanaume thelathini walikusanywa na
kisha kupigwa risasi.
![]() |
| Add caption |
" Waasi hao walikuja karibu saa tatu usiku na kisha kuwakusanya
wanakijiji katika makundi, hususan vijana. Kisha wakaenda nyumba hadi
nyumba na kuwauwa wanaume, na kuchukuwa kila kitu walichokuwa nacho,''
amesema Ali Ndume.
"Wamewauwa watu 106. 105 mia moja na tano ni
wanaume na mwanamke mmoja kikonge aliyekuwa akijaribu kumlinda mjukuu
wake wa kiume. Nadhani alipigwa risasi na kisha akafa."
Kisha wanamgambo hao walienda nyumba hadi nyumba
wakiwauwa watu-wengi wao wakiwa ni wanaume. Baadhi walipigwa risasi
huku wengine wakichinjwa.
Msemaji wa jeshi hakutoa maelezo kuhusu kisa
hicho cha hivi punde lakini ameiambia BBC kwamba jeshi haliwezi kuwa
kila mahali na kusema kuwa wanamgambo hao ni watu wa kuhamahama



0 comments:
Post a Comment