![]() |
| Baadhi ya watu waliofariki Lampedusa |
Serikali ya Utaliana itafanya mazishi ya kitaifa kwa
mamia ya wahamiaji waliokufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria
kuzama katika bahari ya Meditarenia kisiwani Lampedusa wiki jana.
Waziri mkuu Enrico Letta alitoa taarifa hiyo
wakati wa ziara yake kisiwani humo akiambatana na Rais wa tume ya Ulaya
Jose Manuel Barroso.
Bwana Barroso aliahidi kutoa dola milioni 40 kama ufadhili kuwasaidia wakimbizi nchini Utaliana.
Viongozi hao wawili walizomewa walipowasili kisiwani Lampedusa wakiwaita wauaji na wenye kuleta aibu.
Angalau watu 274 wengi wao raia wa Eritrea na
Somalia - walifariki baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama umbali
wa kilomita moja kutoka ufuoni mwa kisiwa cha Lampedusa.
Ilikuwa moja ya majanga mabaya zaidi kuwahi kukumba Utaliana ikihusisha wahamiaji wanaokwenda kutafuta maisha bora barani Ulaya.
Lampedusa ni eneo ambalo hupokea boti nyingi
sana kama hizo na wenyeji wamekuwa wakilalamika kuwa maafisa Utaliana na
katika Muungano wa Ulaya hawajajitahidi katika kutatua tatizo la maelfu
ya wahamiaji kufika katika kisiwa hicho kila mwaka.
Bwana Barroso na Bwana Letta walitembelea kituo
cha muda cha kuhifadhi maiti huku akishika majeneza ya walioangamia.
Baadaye alikutana na waathiriwa walionusurika kifo pamoja na wale
walioendesha shughuli ya uokozi.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja na
waandishi wa habari, Barroso alisema kuwa hatawahi kusahau picha ya
mamia ya majeneza aliyoyaona.


0 comments:
Post a Comment