
Marekani imesema kuwa gaidi aliyekamatwa na vikosi
maalum vya Marekani nchini Libya anzuiliwa katika meli ya kijeshi katika
bahari ya Mediterranea.
Abu Anas al Libi, anadaiwa kuwa na uhusiano na
kundi la kigaidi la al-Qaeda na amekuwa akisakwa kwa kuhusika na
mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Mareakni nchini Kenya na
Tanzania mwaka 1998.
Awali viongozi wakuu wa Libya walitaka maelezo
kutoka kwa Marekani, baada ya Abu Anas al Libi anayedaiwa kuwa mfuasi wa
al-Qaeda kutekwa mjini Tripoli na makamando wa Marekani.
Mwanamme huyo, alikuwa anasakwa kwa kuhusika na
mashambulio dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania miaka
15 iliyopita.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema Anas al Libi sasa anazuwiliwa nje ya Libya.
Kakake amesema kukamatwa kwake kulikuwa kitendo cha uharamia.
Jumamosi makamando wa Marekani piya
walishambulia nyumba mjini Barawe, Somalia, ambayo inadaiwa kutumiwa na
kiongozi mmoja wa kundi la al-Shabaab aliyehusika na shambulio katika
jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi, lakini walishindwa kumpata.
Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Marekani,
John Kerry, amesema kuwa mashambulio hayo mawili yanaonesha dhamira ya
serikali ya Marekani kuwasaka wale wanaohusika na ugaid

0 comments:
Post a Comment