Onika
Tanya Maraj maarufu kama Nicki Minaj member wa Young Money ambaye
amezaliwa miaka 30 iliyopita, anasifika kwa style yake ya kurap na jinsi
anavyojifananisha na mdoli wa barbie. Kitu kingine ambacho Nicki Minaj
anacho ni tatoo ambayo ipo kwenye mkono wa kushoto iliyoandikwa kwa
lugha ya kichina.
So, umewahi kujiuliza nini maana ya tatoo ile ambayo
Nicki Minaj amejichora. Kama ulikuwa hujui ni kwamba hiyo ndiyo tatoo
pekee ambayo Nicki Minaj anayo kwenye mwili wake tofauti na boss wake
Lil Wayne ambaye karibia nusu ya mwili wake una tatoo.
Kwenye
lugha ya kiingereza tatoo hile maana yake ni ”God is always with you”,
kwa kiswahili ni kwamba “Mungu siku zote yupo pamoja nawe”. Sources
zinasema kwamba Nicki Minaj mwenyewe anasema alijichora hiyo tatoo akiwa
na akili za kitoto na kama akiweza kurudi nyuma asingeweza kuichora
tena.
.



