Labels:
BURUDANI,
MICHEZO
Full Time ya Algeria Vs Taifa Stars
Usiku wa November 17 watanzania wengi na
wapenzi wa soka walikuwa wakisubiri kuona mchezo wa pili wa marudiano
wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi kati ya timu ya taifa ya Algeria dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, mchezo ambao ulichezwa Blida Algeria katika uwanja wa Mustapha Tchaker.
Labels:
BREAKING NEWS
‘Ufyatulianaji mkali’ wa risasi Paris
Ufyatulianaji mkali wa risasi
umetokea kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis na ripoti
zinasema operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa
inaendelea.
Maafisa kadha wa polisi wamejruhiwa, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.
Video
iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha
watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi
unusu alfajiri saa za Ufaransa.
Labels:
MATUKIO
Urusi yashambulia Islamic State
Urusi imesema kuwa imetekeleza
shambulio kali zaidi dhidi ya maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wa
Islamic State nchini Syria,ikiwa ni miongoni mwa mashambulizi yake ya
hewani kufikia sasa.
Waziri wa ulinzi Sergei Shoigu,amethibitisha
ripoti za Ufaransa na Marekani kwamba Moscow ilitumia mabomu ya masafa
marefu na makombora .
Labels:
JAMII,
WALIJUA HILI..?
Vatican yawakamata wawili kwa kuvujisha siri
![]() |
| Papa Francis |
Makao makuu ya Papa Vatican imesema
watu wawili imewakamata watu wawili mmoja akiwa kasisi wa kanisa hilo na
mwingine mfanyakazi wa zamani wa makao ya papa kwa tuhuma kuvujisha
nyaraka siri za kanisa hilo.
Wawili hao walikuwa wajumbe wa tume
iliyoundwa na Papa Francis kwa ajili ya jukumu kuleta mabadiliko katika
mfumo wa kifedha wa kanisa katoliki.
Labels:
JAMII,
WALIJUA HILI..?
Wachina kusubiri hadi Machi kupata watoto wawili
![]() |
| Mamlaka ya upangaji uzazi imesema ni lazima sheria ifanyiwe marekebisho kwanza |
Mamlaka kuu inayosimamia upangaji wa
uzazi nchini Uchina imeonya wanandoa nchini humo kwamba sharti
waendelee kutii agizo la kuwa na mtoto mmoja kwenye familia hadi sheria
ifanyiwe marekebisho mwezi Machi.
Alhamisi wiki jana, serikali ilitangaza kwamba ingelegeza sheria na
kuwaruhusu wanandoa kuzaa watoto wawili.
Ilisema uamuzi huo
ulifanywa kutokana na ongezeko kiwango cha wazee ukilinganisha na vijana
katika jamii na lengo ni kuimarisha uchumi.
Labels:
JAMII,
MATUKIO,
WALIJUA HILI..?
Urusi:'Nguvu kutoka nje'ilisababisha ajali ya ndege
![]() |
| Uchunguzi wa vinasa sauti za safari ya ndege unaendelea |
''Nguvu kutoka nje'' ndio
iliyosababisha ajali ya ndege iliyoanguka katika rasi ya Sinai na kuua
watu 224 wengi wao raia wa Urusi.
Kogalymavia, Kampuni inayomiliki
ndege hiyo ya Urusi imesema hakuna njia nyengine ya kuelezea ajali hiyo
mbaya zaidi katika miaka ya hivi punde.
Katika mkutano na
wanahabari jijini Moscow, afisa mmoja mkuu wa shirika hilo Kogalymavia
alipinga madai kuwa ndege hiyo ilikuwa na hitilafu au makosa ya rubani.
Labels:
JAMII,
MATUKIO
Polisi 4 washtakiwa kwa kuua mshukiwa
![]() |
| Polis 4 washtakiwa kwa kuua mshukiwa |
Maafisa wanne wa polisi wameshtakiwa
baada ya kunaswa na kamera za siri (CCTV) wakimpiga risasi na kumuua
mshukiwa mmoja wa uhalifu
Gazeti mmoja la Afrika Kusini, Sunday
Times lilichapisha video hiyo iliyowaonesha maafisa hao wakimpiga risasi
na kumuua mshukiwa wa uhalifu licha ya kuwa alikuwa amejisalimisha kwa
polisi.
Afisa mwengine wa polisi anaonekana akimvurumishia mateke
katika tuko hilo lililotokea katika barabara ya Krugersdorp city,
Magharibi mwa Johannesburg
Labels:
JAMII,
MATUKIO,
WALIJUA HILI..?
Amkimbia mume, aenda kuchumbiwa
| Elizabeth Kinyami anayedaiwa kumtoroka mumewe. |
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini Robert
alifiwa na mkewe wa kwanza ambaye alizaa naye watoto wawili, lakini
wakati akiwa naye, alikuwa akichepuka na Elizabeth, hivyo baada ya
mwenzake kutangulia mbele ya haki, alimchukua mchepuko wake na kuishi
naye kinyumba.
Inadaiwa kuwa baada ya kuishi kama mke
na mume kwa miaka miwili, msichana huyo alimwambia Robert kuwa amepata
chuo cha kusoma mjini Tanga, ambapo mwanaume alikubali na kumsaidia ili
aendelee na masomo
Labels:
MATUKIO,
WALIJUA HILI..?
Kenya yaanzisha operesheni kuzima Alshabab
![]() |
| Rais Kenyatta alimuagiza inspekta mkuu wa polisi kuendesha operesheni dhidi ya ugaidi |
Operesheni hiyo inayoendeshwa na
vikosi maalum vya kupambana na ugaidi kwa ushirikiano na jeshi la taifa
linalenga wapiganaji takriban mia tatu wa Jeysh al Ayman wanaosadikika
kujificha katika msitu huo. Kundi hilo la Jeysh al Ayman linasadikiwa
kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Al Shabaab
Labels:
JAMII,
MATUKIO
Mama Mpalestina aliyechomwa aaga dunia
Mwanamke mmoja wa kipalestina
amekufa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa shambulio mwezi Julai
lililomuua mumewe na mtoto wao mdogo wa kiume.
Riham Dawabsha
alikua anauguza majeraha ya kuungua kiasi cha asilimia tisini ya mwili
wake aliyoyapata baada ya nyumba yao kupigwa na mabomu ya moto katika
kijiji cha Duma kilichopo katika ukingo wa magharibi .
Shambulio hilo linaaminiwa kufanywa na walowezi wa kiyahudi
Labels:
JAMII,
MATUKIO
Ujerumani na ongezeko la wahamiaji
![]() |
| Polisi wa Ujerumani akizungumza na wahamiaji |
Serikali ya Ujerumani imetangaza hatua kadhaa zitakazotumiwa kuisaidia kukabiliana na ongezeko la wahamiaji
Miongoni mwa hatua hizo, ni kutoa kiasi cha fedha dola bilioni tatu kusaidia serikali za majimbo na manispaa.
Pia
imeamua kuharakisha mchakato wa kupitia maombi ya wanaotaka hifadhi,
kutoa nyumba na kutenga
Subscribe to:
Comments (Atom)









