![]() |
| Mamlaka ya upangaji uzazi imesema ni lazima sheria ifanyiwe marekebisho kwanza |
Mamlaka kuu inayosimamia upangaji wa
uzazi nchini Uchina imeonya wanandoa nchini humo kwamba sharti
waendelee kutii agizo la kuwa na mtoto mmoja kwenye familia hadi sheria
ifanyiwe marekebisho mwezi Machi.
Alhamisi wiki jana, serikali ilitangaza kwamba ingelegeza sheria na
kuwaruhusu wanandoa kuzaa watoto wawili.
Ilisema uamuzi huo
ulifanywa kutokana na ongezeko kiwango cha wazee ukilinganisha na vijana
katika jamii na lengo ni kuimarisha uchumi.
Lakini maafisa wamesema sera ya kuwa na mtoto mmoja katika familia itaendelea kutekelezwa hadi sharia ifanyiwe mabadiliko.
Mnamo
Ijumaa, afisa mmoja alinukuliwa akisema kwamba wajawazito walio na
mimba ya watoto wa pili hawataadhibiwa tena, jambo lililodokeza kwamba
sera hiyo tayari ilikuwa imeanza kutekelezwa.
Lakini Jumapili Tume
ya Kitaifa ya Afya na Upangaji Uzazi ilisema maafisa wa serikali
wataendelea kutekeleza sharia hizo hadi sharia ifanyiwe marekebisho
Machi.
"Sera ya kuruhusu watoto wawili sharti itekelezwe kwa mujibu wa sheria,” afisa wa tume hiyo alisema kupitia taarifa.
Hadi
sera hiyo mpya iidhinishwe kisheria, maafisa wa serikali “lazima
waendelee kutekeleza sera iliyopo sasa”, taarifa hiyo ilisema.
Serikali
inakadiria kwamba familia 90 milioni zitapata nafasi ya kuongeza mtoto
mwingine, sera ya kuwa na watoto wawili ikianza kutekelezwa.


0 comments:
Post a Comment