![]() |
| Papa Francis |
Makao makuu ya Papa Vatican imesema
watu wawili imewakamata watu wawili mmoja akiwa kasisi wa kanisa hilo na
mwingine mfanyakazi wa zamani wa makao ya papa kwa tuhuma kuvujisha
nyaraka siri za kanisa hilo.
Wawili hao walikuwa wajumbe wa tume
iliyoundwa na Papa Francis kwa ajili ya jukumu kuleta mabadiliko katika
mfumo wa kifedha wa kanisa katoliki.
Uongozi wa juu wa kanisa hilo
unaamini kwamba wawili hao walivujisha nyaraka muhimu za majadiliano ya
tume hiyo kwa waandishi habari wanaofanya uchunguzi wa masuala ya
rushwa ndani ya Vatican.
Nyaraka hizo ndizo zitakazotumika
kuchapisha vitabu viwili vinavyotarajiwa kutolewa kuhusiana na utata wa
hali ya kifedha wa Vatican.mmoja wa waandishi habari Gianluigi Nuzzi
ambaye alichapisha moja ya nyaraka hizo mnamo mwaka 2012 ambaye anadai
kupewa nyaraka hizo na mtangulizi wa Papa Francis


0 comments:
Post a Comment