Waziri wa mambo ya nje wa Syria , Walid Maullem,
amesema anapinga vikali madai kuwa wanajeshi wa serikali ya Syria
walitumia silaha za kemikali.
Maullem, aliyasema hayo mjini Damascus, baada ya
Marekani kudai kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa silaha
za kemikali zilitumika nchini humo.
Bwana
Maullem,
amesema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, wameshindwa kufika
katika eneo la pili linalodaiwa kushambuliwa kwa silaha hizo, baada ya
kuzuiliwa na wapiganaji wa waasi.
Marekani na washirika wake wanajadili uwezekano
wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria kufuatia madai ya shambulio hilo
la kemikali lililotokea wiki iliyopita
Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari, kuwa ikiwa nchi yake
itashambuliwa kijeshi, kwa misingi ya kuwepo kwa silaha za kemikali,
itakuwa kwa visingizio vya uongo na jambo ambalo halina msingo wowote.
Amekariri kuwa serikali ya Syria imetimiza ahadi
zote ilizotoa kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuruhusu wachunguzi
wake kufika nchini humo na pia kuwapa ulinzi
Awali serikali za Urussi na Uchina, kwa mara
nyingine tena zimetoa onyo dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutatua
mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Syria.
Onyo hilo limetolewa huku Marekani na washirika
wake wakijadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria,
kujibu shambulio lililotokea wiki iliyopita

0 comments:
Post a Comment