![]() |
| Rais Kenyatta alimuagiza inspekta mkuu wa polisi kuendesha operesheni dhidi ya ugaidi |
Operesheni hiyo inayoendeshwa na
vikosi maalum vya kupambana na ugaidi kwa ushirikiano na jeshi la taifa
linalenga wapiganaji takriban mia tatu wa Jeysh al Ayman wanaosadikika
kujificha katika msitu huo. Kundi hilo la Jeysh al Ayman linasadikiwa
kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Al Shabaab
Msemaji wa shirika la
msalaba mwekundu katika eneo la Lamu na Kilifi Bwana Musa Hassan,
ameliambia gazeti la The Standard kuwa asilimia kubwa ya watu
wanaotoroka ni wakaazi wa eneo la Basuba na wengine walioko Kusini mwa
Garissa wanaohofia kupatikana katikati ya makabiliano yanayotarajiwa
kati ya wanamgambo hao na vikosi vya usalama vya Kenya.
Wizara ya
usalama ilitoa ilani mwishoni mwa juma ikiwataka wakaazi wa maeneo
yanayopakana na msitu huo ikiwataka watu wote wanaomiliki bunduki katika
eneo hilo kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo
inayohusisha vikosi vya wanahewa na wale wa nchi Kavu.
![]() |
| Majuzi tu kundi hilo linadaiwa kuvamia wanakijiji wa Basuba |
Tayari idadi kubwa ya vikosi vya jeshi vimeripotiwa kuonekana katika
maeneo ya Mangai, Baure,Kaskazini mwa Lamu, Bodhai na Hulugho.
Mkuu
wa polisi katika eneo la Ijara Christopher Rotich amenukuliwa
akithibitisha kuwepo kwa mipango hiyo ya kudhibiti utovu wa usalama
unaotokana na mashambulio ya mara kwa mara yanayodaiwa kutekelezwa na
kundi hilo la wanamgambo la wa Jeysh al Ayman.
Kundi hilo lanalosemekana kujumuisha wenyeji linalaumiwa kwa jaribio la kuvamia kambi ya kijeshi iliyoko Baure mwezi juni.
Aidha kundi hilo ndilo linalodaiwa kutekeleza shambulizi la bomu la kutegwa ardhini mapema mwaka huu.
![]() |
| Manuari za kijeshi zilionekana zikiingia Boni |
Majuzi tu kundi hilo linadaiwa kuvamia wanakijiji wa Basuba na kutoa
hutuba kwa muda mrefu mbali na kuwaonya wenyeji dhidi ya kutoa habari na
kushirikiana na polisi.
Inspekta mkuu wa polisi wa Kenya, Joseph
Boinnet, alitangaza hali ya tahadhari katika maeneo ya msitu wa Boni
huku akitoa amri ya kuitangaza Boni kuwa eneo la Operesheni.
Msitu huo mkubwa wa Boni upo katika majimbo tatu nchini Kenya ya Lamu, Garissa na Tana River.
Aidha unapakana na bahari Hindi kuanzia Lamu hadi mpaka wa Kenya na Somalia.




0 comments:
Post a Comment