| Amina Mohammed amesema kwa kuwa Kenyatta ni rais hali inabadilika kuhusu ICC |
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed
amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye mamlakani amewahi kufikishwa
mbele ya mahakama ya ICC. Taarifa hii bila shaka imetafsiriwa na wengi
kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru Kenyatta kuwasilishwa mbele
ya mahakama ya ICC mwezi ujao.
Duru zinseama kuwa kuwa hofu kuwa huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama.
Waziri Amina amesema kuwa Rais
Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa
yeye ni rais hali imebadilika. Kenyatta anatakikana na mahakama ya ICC
kuhusiana na uhalifu dhidi ya bindamu katika ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu mwaka 2007/2008
Bi Abdalla aliyasema hayo kwenye mkutano na
waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika
kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.
Wakati huohuo, Kenya imekanusha madai kuwa
inashinikiza mataifa mbalimbali ya Afrika kujiondoa katika mkataba wa
Roma uliobuni mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC.
Waziri wa mashauri ya kigeni nchini humo balozi
Amina Mohamed kuwa Kenya imekuwa ikishirikiana na mahakama hiyo na hata
Naibu wa Rais William Ruto kwa sasa yuko mjini the Hague kuhudhuria
vikao vya hakama hiyo.
Matamshi ya Bi Amina yanatukia siku chache tu
kabla ya mkutano wa Marais wa Afrika utakaofanyika Ethiopia jumamosi
hii. Bi Amina alisema kuwa Kenya haijashinikiza nchi yoyote kuondoka
kwenye mkataba wa Roma na kuwa mkutano wa AU umeitishwa na nchi mbili
tofauti wala sio Kenya.
Kadhalika Amina amesema kuwa Kenya haina nia yoyote ya kutoendelea kushirikiana na mahakama ya ICC.
Wakati huohuo mwanasheria mkuu wa Kenya Githu
Muigai amepewa fursa ya kuielezea mahakama ya ICC kwa nini bunge la
Kenya lilipitisha hoja ya kuitaka Kenya kujiodnoa kutoka katika mkataba
wa Roma.
Majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya naibu rais wa
Kenya William Ruto, walisema kuwa maelezo ya Muigai yatasaidia mahakama
kuchukua hatua zaidi za kuwalinda mashahidi ambao tayari wametoa
ushahidi wao.
Jaji mkuu anayeongoza jopo la majaji
wanaosikiliza kesi dhidi ya Ruto, Chile Eboe-Osuji,ambaye alielezea
kuwa wanajadili swala hilo na kuwa maelezo ya Muigai kuhusu mkakati wa
serikali kutaka kuiondoa Kenya kutoka katika mahakama ya ICC utawasaidia
kufanya uamuzi.

0 comments:
Post a Comment